Na Mwandishi wetu, Moshi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameagiza uongozi wa Kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha Karanga kutafuta masoko ndani na nje ya nchi Pamoja na kuandaa mikakati ya mauzo ambayo itahakikisha ukuaji wa soko na uuzwaji wa bidhaa za ngozi zitakazo zalishwa kiwandani hapo.

Mhe. Mhagama ametoa ushauri huo alipofanya ziara ya ufuatiliaji wa ujenzi wa kiwanda. hicho Agosti 13,2020.

“Ni matarajio yangu kuwa watendaji kwa kushirikiana na idara ya masoko mna mikakati madhubuti ambayo itawafanya muweze kuwa wabunifu katika kuzalisha bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa ili bidhaa hizo ziuzike katika soko la ndani na nje ya nchi, msisubiri uzalishaji uanze ndio muanze kutafuta masoko hayo” alishauri Mhe. Mhagama

Waziri Mhagama ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambalo alilitoa mwaka 2016 kwa kuelekeza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye miradi yenye tija.

” Ili azma yetu itimie, PSSSF na Jeshi la Magereza ongezeni kasi na nguvu ya ujenzi katika hatua hii ya pili ya mradi huu ili kiwanda kikamilike kwa wakati”alielekeza Mhe. Waziri.

Alisema kiwanda hiki ni ndoto yetu, kikikamilika kwa kusimamiwa. vyema, kitakuwa cha mfano katika eneo la Afrika Mashariki, ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na barani zima la afrika kutokana na bidhaa bora zitakazozalishwa kiwandani na kiwanda cha Karanga.

“Naomba uongozi wa kiwanda uhakikishe malengo yote yanatimia na kiwanda kinaanza kufanya kazi ya uzalishaji mapema,” aliagiza Mama Mhagama.

Aidha Waziri Mhagama alifafanua kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imejipanga kufanya majadiliano ya karibu na Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Idara ya Uwekezaji, Taasisi na Vyuo vya Mafunzo ili kuhakikisha kiwanda kinakuwa na soko la ndani la uhakika.

Pia Mhe Mhagama alitoa maagizo kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha anasimamia mikataba yote ya mradi huo ili kila jambo lolote lililopangwa kutekelezwa katika mradi huo likamilike kwa wakati.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe alisema kuwa kiwanda hicho ni muhimu na kitasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa taifa pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa wingi.

Mkurungenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba alisema PSSSF itazingatia maagizo yote yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri, kama wabia wa mradi huo.

” Hadi sasa mitambo ya kuchakata ngozi imeshawasilishwa kiwandani na karibuni wataalam kutoa nchini Italia watawasili kwa ajili ya kuisimika mitambo hiyo pamoja na kutoa mafunzo elekezi kwa wataalum wa ndani katika kiwanda hicho” alifanunua Bw. Kashimba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Mhandisi Masud Omari amesema tayari wameshaanza kufungua maduka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoani Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza, alisema watafungua duka katika makao makuu ya nchi jijini Dodona hivi karibuni.

“Nia yetu pia ni kutafuta mawakala wenye uzoefu wa kuuza na kusambaza bidhaa za ngozi ndani na nje ya nchi.

Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha karanga kinaendeshwa kwa ubia kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Wasimamizi wa mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga alipotembelea kiwanda hicho kukagua maendeleo ya ujenzi. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Wasimamizi wa mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga alipotembelea kiwanda hicho kukagua maendeleo ya ujenzi. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akieleza jambo wakati wa kikao kifupi cha upokeaji wa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga.

Mkurungenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kuwasili kiwandani hapo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo. Wa kwanza Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Mhandisi Masud Omar.

Muonekano wa baadhi ya Majengo ya Kiwanda hicho yaliyojegwa katika awamu ya kwanza (LOT 1) yakiwa yamekamilika.

Sehemu ya Mitambo ambayo itasimikwa katika majengo yaliyokamilika katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda cha Karanga kilichopo Mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya Mafundi wakisuka ndondo katika maeneo eneo moja wapo la awamu ya pili ya ujenzi ya kiwanda hicho cha kuchakata Ngozi kilichopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (wa pili kutoka kushoto) akiwa ameambatana pamoja na Wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi alipokuwa akigagua maendeleo ya mradi huo uliopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkurungenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba.

Mratibu Msaidizi ambaye pia ni Mhandisi wa Umeme, Paul Kiweri (kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (wa nne kutoka kulia) walipotembelea eneo la usambazaji mifumo ya umeme “Power House” katika kiwanda hicho.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (katikati) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi alipokuwa akigagua maendeleo ya mradi huo uliopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (katikati) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi alipokuwa akigagua maendeleo ya mradi huo uliopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.