FAQ’s2019-10-09T14:47:03+00:00
Mwanachama wa PSSSF ni nani?2019-09-12T14:33:42+00:00

Kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 waliokuwa wanachama wa mifuko iliounganishwa yaani PPF, PSPF, LAPF na GEPF waliohamishiwa katika mfuko wa PSSSF wataendelea kuwa wanachama na kuchangia katika Mfuko wa PSSSF. Watumishi wapya watakaoajiriwa kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 katika utumishi wa Umma, mashirika ya umma na makampuni yote ambayo serikali inamiliki zaidi ya asilimia 30 ya hisa watatakiwa kusajiliwa na kuchangia katika mfuko wa PSSSF. Wanachama wa mfuko ni pamoja na wastaafu na wategemezi waliokuwa wanalipwa pensheni na mifuko iliounganishwa.

Ili mtumishi awe mwanachama wa PSSSF anapaswa awe na sifa gani?2019-09-12T14:37:58+00:00

Pamoja na sifa zilizotajwa awali, mtumishi anapaswa kuwa na kitambulisho cha uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho Tanzania (NIDA).

Je kama Mwanachama hana kitambulisho cha Uraia atakosa stahiki zake katika Mfuko?2019-09-13T07:03:46+00:00

Hapana. Taarifa zako zitakuwa katia Mfuko, lakini utapaswa kwenda kujiandikisha ili uweze kupata huduma zako kwa wakati bila ususmbufu. Inategemewa ifikapo Juni 2019 wanachama wote wa PSSSF watakuwa na namba ya utambulisho ya NIDA amabayo itawasilishwa kwa mwajiri ambaye atakuwa anaitumia katika kuwasilisha michango.

Je ni jukumu la nani kuhakikisha michango ya wanachama inawasilishwa?2019-09-13T07:12:40+00:00
  1. Mwajiri, kuhakikisha anakata kwenye mshahara wa mtumishi sehemu inayotakiwa kísheria, kujumuisha na sehemu ya mwajiri na kuwasilisha kwenye Mfuko kiasi chote kinachotakiwa si zaidi ya siku 30 tangu kuisha kwa mwezi wa makato hayo.
  2. Mwanachama, kuhakikisha katika hati yako ya mshahara kuna makato ya PSSSF Kama hayapo toa taarifa haraka kwa mwajiri ili arekebishe dosari hiyo.
  3. Mfuko wa PSSSF, kufanya ufatiliaji wa mara kwa mara kuhakikisha michango inawasilishwa kwa wakati.
Ofisi za PSSSF zipo wapi?2019-09-13T07:24:55+00:00

Katika kuhakikisha hudumaza Mfuko zinawafikia watanzania wote, PSSSF ina ofisi katika mikoa 28 Tanzania Bara (ikiwa ni pamoja na mikoa mitatu ya kimkakati ya llala, Kinondoni na Temeke katika mkoa wa Dar es Salaaam). Pia tuna ofisi Tanzania Visiwani (Unguja na Pemba).

Huduma za PSSSF kwa wanachama wake zinalipiwa?2019-09-13T07:29:45+00:00

Hapana. Huduma kwa wanachama wa PSSSF hazilipiwi bali hutolewa bure, huduma hizo ni pamoja na uhakiki wa taarifa za michango ya wanachama, wastaafu na ufuatiliaji wa huduma nyingine. Katika hili wanachama wanapaswa kuzingatiakwamba huduma za Mfuko zinatolewa bila malipo na watumishi ambao wana vitambulisho vya Mfuko kuwatambulisha. Mawasiliano yote kwa wanachama yatakuwa yakitolewa na Afisa wa Mfuko au kupitia mawasiliano rasmi ya PSSSF. Mwanachama anapoombwa fedha kwa ajili yeyote ile, asitoe. Anachopaswa kufanya ni kutoa taarifa katika kituo cha polisi au ofisi ya PSSSF iliyo karibu nae.

Kwanini PSSSF inafanya uhakiki wa wastaafu wanaodai stahiki zao?2019-09-13T07:31:06+00:00

Zoezi la uhakiki wa ziada linafanyika kwa wastaafu ambao taarifa zao hazijakamilika ikiwa ni pamoja na waliosimamishwa kazi kwa mujibu wa Sheria, kwa ajili ya kuhakiki vyeti na wote wenye kesi za nidhamu na jinai. Hawa wote watalipwa ndani ya muda uliopangwa yaani Januari 2019 baada ya uhakiki kukamilika Uhakiki wa wastaafu na wategemezi wanaopata pensheni ni jambo la kawaida na lengo lake ni kuhakikisha Mfuko unazo kumbukumbu sahihi za wastaafu wake na kwamba pensheni inalipwa kwa mlengwa halisi.

Mwanachama anaweza kuwasiliana vipi na PSSSF?2019-09-13T07:35:21+00:00

Wanachama anaweza kufika katika ofisi zetu zilizopo katika kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, pia wanaweza kuwasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo 0800 110 055, 0800 110 040. Kupiga namba hizo ni bure.

Je Mwanachama wa Mfuko akiacha kazi anaweza kulipwa mafao ya kujitoa?2019-09-13T07:37:21+00:00

Hapana. Mwanachama wa PSSSF akiacha kazi kwa hiari yake hatapata mafao hadi atakapofikisha umri wa kustaafu kisheria Atashauriwa kuendeleza uchangiaji wake akiwa kwenye ajira nyingine. Kama akiwa ameachishwa kwa sababu nyingine yeyote bila hiari yake, Mfuko utamlipa mafao ya kukosa ajira kwa kipindi cha miezi 6, mafao hayo yatasita endapo atapata kazi kabla ya kuisha kwa miezi hiyo sita. lkipita miezi 18 baada ya kwisha kipindi cha kupata fao la kukosa ajira, mwanacharma anaweza kuomba michango yake kwenye mfuko kuhamishiwa kwenye Mfuko wa hiari. Michango itahamishwa baada ya kuondoa jumla ya fao la kukosa kazi. Fao la kukosa kazi litalipwa si zaidi ya mara tatu katika utumishi wote wa wanachama.

Go to Top