Kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 waliokuwa wanachama wa mifuko iliounganishwa yaani PPF, PSPF, LAPF na GEPF waliohamishiwa katika mfuko wa PSSSF wataendelea kuwa wanachama na kuchangia katika Mfuko wa PSSSF. Watumishi wapya watakaoajiriwa kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 katika utumishi wa Umma, mashirika ya umma na makampuni yote ambayo serikali inamiliki zaidi ya asilimia 30 ya hisa watatakiwa kusajiliwa na kuchangia katika mfuko wa PSSSF. Wanachama wa mfuko ni pamoja na wastaafu na wategemezi waliokuwa wanalipwa pensheni na mifuko iliounganishwa.