Hapana. Mwanachama wa PSSSF akiacha kazi kwa hiari yake hatapata mafao hadi atakapofikisha umri wa kustaafu kisheria Atashauriwa kuendeleza uchangiaji wake akiwa kwenye ajira nyingine. Kama akiwa ameachishwa kwa sababu nyingine yeyote bila hiari yake, Mfuko utamlipa mafao ya kukosa ajira kwa kipindi cha miezi 6, mafao hayo yatasita endapo atapata kazi kabla ya kuisha kwa miezi hiyo sita. lkipita miezi 18 baada ya kwisha kipindi cha kupata fao la kukosa ajira, mwanacharma anaweza kuomba michango yake kwenye mfuko kuhamishiwa kwenye Mfuko wa hiari. Michango itahamishwa baada ya kuondoa jumla ya fao la kukosa kazi. Fao la kukosa kazi litalipwa si zaidi ya mara tatu katika utumishi wote wa wanachama.