Msemaji Mkuu wa serikali, Dkt Hassan Abbasi, amewasihi Watumishi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake.

Dkt Abbas amesema hayo alipotembelea makao makuu ya PSSSF jijini Dodoma alipokwenda kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Bw. Hosea Kashimba.

Dkt. Hassan Abbasi (Kushoto) akimkabidhi jarida la Nchi Yetu Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya PSSSF jijini Dodoma, kulia ni Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi.

“Tunaona kazi kubwa na nzuri mnayofanya, naomba mwendelee kuhudumia vyema wanachama wenu, hususani Wazee wetu ambao wamelitumikia taifa letu” alisisitiza Dkt. Abbasi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Kashimba alisema Baada ya Mifuko kuunganishwa, PSSSF imeboresha huduma kwa wanachama katika maeneo mbalimbali.

“Baada ya kuungana tumeboresha sana maeneo yafuatayo; utunzaji wa kisasa wa kumbukumbu za wanachama ambapo sasa taarifa za wanachama zinapatikana katika za PSSSF popote nchini, Mfuko una vituo vya huduma kwa wateja maalum kwa kutoa huduma kwa wanachama na Mfuko una ofisi katika kila mkoa Tanzania. Pia wanachama anaweza kuwasiliana nasi kwa kupiga simu ya bure kupitia namba 0800 110 040” alifafanua Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF.

PSSSF ilianza rasmi kutoa huduma kwa wanachama wake Agosti 1, 2018 baada ya kuunganishwa wa iliyokuwa mifuko ya LAPF, PPF, GEPF na PSPF.

Mkurugenzi wa Idara ya habari maelezo na Msemaji Mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika mazungumzo na
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba.

Mkurugenzi wa Idara ya habari maelezo na Msemaji Mkuu wa serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika mazungumzo na
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba.