Na Mwandhishi Wetu, Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)  Bw. Hosea Kashimba mnamo tarehe Februari 24, 2020 alifanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu alikutana na kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee kwa lengo la kuzungumzia uwekezaji unaofanywa kwa pamoja kati ya PSSSF na Jeshi la magereza katika kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga kilichopo Moshi, Kilimanjaro.

Uwekezaji katika kiwanda hiki umejumuisha ukarabati wa kiwanda cha zamani na ujenzi wa kiwanda kipya. Ukarabati wa Kiwanda cha zamani umekamilika na uzalishaji umeanza na kiwanda kinazalisha jozi 400 kwa siku ambazo wateja wake wakubwa ni majeshi ya Tanzania pamoja na wananchi wa kawaida. Ujenzi wa kiwanda kipya upo katika hatua  za mwisho.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Hosea Kashimba (kulia) akiwa na Kamishina Jenerali wa Magereza Bw.Suleiman Mzee.