Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Bw. Hosea Kashimba amefanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto na kumhakikishia kuwa wakati wote Mfuko upo tayari kutoa huduma kwa Jeshi la Polisi na wanachama wote.

Kamanda Muroto akimwonesha taarifa za mwanachama mmoja kupitia simu yake ya mkononi.

“PSSSF tumeshafanya kikao na viongozi wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na wakuu wa majeshi yote yaliyo chini ya wizara hiyo, lengo kwa baadae ni kutoa elimu kwa askari juu ya namna gani ya kujindaa vyema kwa ajili ya kustaafu, nina hakika tutawafikia askari wako wa Dodoma,” alifafanua Bw. Kashimba.

Kamanda Muroto akiwa katika mazungumzo na Bw. Kashimba pamoja na Maafisa wengine wa Mfuko, Rehema Mkamba (kushoto) na Abdul Njaidi.

Kwa upande wake Kamanda Muroto alisema Jeshi la Polisi Dodoma lipo imara na kwamba linaendelea kukabiliana na kudhibiti uhalifu kwa lengo la kuhakikisha usalama kwa wakazi wa Dodoma pamoja na watumishi wa PSSSF.

“Jiji lipo salama, fanyeni kazi kwa kujiamini na amani, sisi tupo kazini masaa 24. Lakini PSSSF muwe tayari kuwahudumia wanajeshi wangu ili wastaafu kwa amani, alisisitiza kamanda Muroto.

Kamanda Muroto akipokea zawadi kutoka PSSSF.

Mkurugenzi mkuu wa Mfuko, amekuwa akifanya ziara mbalimbali za kikazi kwa watendaji Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu akifurahia jambo na Kamanda Muroto, wengine pichani ni Maafisa wa Polisi na PSSSF.