Bodi ya wadhamini ya PSSSF imetembelea miradi ya PSSSF iliyoko Dar es salaam kuanzia Disemba 12 hadi 14. Katika
ziara hiyo mwenyekiti wa bodi Mussa Iyombe ameridhishwa na miradi iliyopo na kusisitiza kuongeza juhudi katika
kujitangaza zaidi kwa lengo la kuongeza wateja. Katika ziara hiyo Bodi ilitembelea mradi wa viwanja vya Kimbiji, Kiga-
mboni, PSSSF House, PSSSF /NHC IPS building, Ubungo Plaza, pamoja na mradi wa APC Hotel and Conference Centre

Wajumbe wa Bodi ya PSSSF wakiwa Katika mradi wa viwanja vya Kimbiji, Kigamboni Jijini Dar es Salaam,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Mussa Iyombe.

Mradi wa APC Hotel and Conference  ni wa ubia kati ya PSSSF na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) una ukumbi wenye uwezo wa kuchukua watu 1,200 kwa wakati mmoja, kumbi 3 ndogo za mikutano, mgahawa na kumbi mbili kubwa za kakakuona  na Kiboko. 

Katika mradi huo kuna hosteli yenye vyumba 96 vya kawaida, 6 vya hadhi ya kati na 6 vya hadhi ya juu. Pia katika mradi huo kuna sehemu ya kufanyia mazoezi na pia burudani mbalimbali. APC Hotel and Conference Centre kuna mgahawa unaweza kutoa huduma ya chakula wakati wote wa semina na mikutano mbalimbali.

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Mhandisi Mussa Iyombe ametoa rai kwa uongozi wa APC Hotel and Conference  kuhakikisha wanajitangaza hususani kwa taasisi za Serikali ili waweze kujua huduma mbalimbali zinazotolewa kwa lengo la kuongeza wateja kwa mradi huo. Mradi huo upo Bunju, jijini Dar es Salaam.

Moja ya kumbi katika APC Hotel and Conference Centre ambalo hutumika kwa ajili ya mikutano na shughuli mbalimbali.

Wajumbe wa Bodi wakimsikiliza Meneja wa kengo la IPS Bw. Itika Mwakangale walipotembelea mradi huo ulipo jijini Dar es Salaam.