Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Bodi ya zabuni ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ipo mjini Morogoro kwa ajili ya kuogezewa ujuzi ili iweze kutenda kazi zake kwa weledi na ufanisi.

Wajumbe wa Bodi ya zabuni ya PSSSF wakiwa katika picha ya pamoja na Mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Aziz Kilonge (katikati, mstari wa mbele).Wajumbe hao wapo mjini Morogoro wakihudhuria mafunzo.

Akizungumzia mafunzo hayo, Katibu wa bodi hiyo Bw. Ernest R. Khisombi alisema, mafunzo hayo ni ya kawaida kwa wajumbe wa bodi ya zabuni, mafunzo ni ya siku tatu, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Machi, 2021 na yanafanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

“Mafunzo hayo yanaendeshwa na Bodi ya Watalaamu wa Ununuzi na Ugavi juu ya Utekelezaji wa Ununuzi wa Umma kwa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011, Kanuni zake za mwaka 2013 kama zilivyoboreshwa mwaka 2016, 2018 na 2019. Lengo likiwa ni kuwawezesha wajumbe kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi” alifafanua Katibu wa bodi hiyo Bw. Ernest R. Khisombi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi.

Mkufunzi wa mafunzo hayo ni Bw. Aziz Kilonge, mshauri mwelekezi na galacha wa Ununuzi na Ugavi, Bw. Aziz, amefanya kazi hizo kwa zaidi ya miaka 20.

Bodi ya Zabuni inaongozwa na Mwenyekiti, Bw. Gilbert Chawe na ina wajumbe sita; Bw.Fortunatus Magambo, Bibi. Beatrice Musa-Lupi, Bw. Paul Kijazi, Bw. Abdul Njaidi, Bw. Victor Kikoti na Bibi. Laila Maghimbi na Bw. Ernest R. Khisombi ambaye ni Katibu wa Bodi.

Matukio katika Picha:

Wajumbe wa Bodi ya zabuni ya PSSSF wakiendelea na mafunzo.

Katibu wa Bodi ya zabuni, Bw. Ernest R. Khisombi (kushoto) na Mjumbe Bw. Victor Kikoti wakifuatilia mafunzo hayo.

Bibi. Laila Maghimbi, Bw. Abdul Njaidi (wajumbe wa Bodi) na Bibi Gloria Nguve kutoka kurugenzi ya Ununuzi na Ugavi wakifuatilia mafunzo hayo (Picha zote: PSSSF).