*Imeridhika na maendeleo ya mradi

*Yaelekeza Menejimenti kufuatilia kwa karibu

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

BODI ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) walitembelea mradi wa machinjio ya kisasa ya nyama ya Nguru yaliyopo Morogoro kwa lengo la kuona hatua za utekelezaji wa mradi huo.

Katika ziara hiyo, Bodi ya Wadhamini  wa PSSSF, imeridhirika  na maendeleo ya mradi na kuiagiza menejimenti ya Mfuko iendelee kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ambao una faida na tija kwa Mfuko na taifa kwa jumla.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamie kwa Watumishi wa Umma (Pichani) wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha nyama cha Nguru kilichopo Mvomero, Morogoro

Ujumbe huo wa   Bodi uliongozwa na Makamu Mwenyeki wake, Dkt. Aggrey Mlimuka na Menejimenti iliogozwa na Mkurugezi wa Mfuko, CPA. Hosea Kashimba. Wajumbe hao walitembelea kiwanda hicho Aprili 17, 2021.

Kiwanda cha nyama cha Nguru kilichopo eneo la Nguru, Mvomero-Morogoro kinamilikiwa na Mfuko wa PSSSF kwa asilimia 39, Eclipse Investment kwa asilimia 46 na Busara Investment LLP kwa asilimia 15. katika kiwanda hiki ambacho ni machinjio ya mifugo (Mbuzi na Ng’ombe). Katika kiwanda hiki, mifugo itanenepeshwa katika ranchi hiyo, kabla ya kuchinjwa kwa ajili ya soko la ndani na nje hususan nchi za Mashariki ya Kati.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamie kwa Watumishi wa Umma (Pichani) wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha nyama cha Nguru kilichopo Mvomero, Morogoro.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamie kwa Watumishi wa Umma (Pichani) wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha nyama cha Nguru kilichopo Mvomero, Morogoro.