Ofisi ya Waziri Mkuu imeutaka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma PSSSF na Jeshi la Magereza, wanaotekeleza kwa ubia mradi wa Ujenzi wa kiwanda kipya cha viatu na bidhaa za ngozi katika gereza la karanga, Moshi Mkoani Kilimanjaro, wenye thamani za zaidi ya bilioni za Kitanzania 75.3 kufanya kazi mchana na usiku kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kama ilivyo kwenye mkataba wa ujenzi unaoelekeza kukamilika mradi huo Februari mwaka 2020 kutokana na umuhimu wake ambapo ajira takriban 7,000 zinatarajiwa kuzalishwa.

Akiwa katika muendelezo wake wa kutembelea miradi iliyokwisha kutekelezwa na inayotekelezwa na PSSSF, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, JENISTER MHAGAMA, amezitaka pande zote kutimiza wajibu wake na kutaka kupewa mpango kazi ili kuondoa visingizio kwenye utekelezaj mradi huo muhimu kwa maendelea ya nchi hususan kwa wananchi wa Kilimanjaro na Mikoa ya jirani, ambapo jumla ya ajira 3,000 za moja kwa moja na 4,000 zisizo za moja kwa moja zitazalishwa huku pia likiwa ni soko la uhakika la ngozi zilizokuwa zinatupwa na wafugaji, nakutarajiwa kuzalisha jozi za viatu 4,000 kwa siku takribani jozi milioni 1.2 kwa mwaka.

Kiwanda hicho kipya ni upanuzi wa kiwanda kilichopo sasa gerezani hapo,kinachozalisha jumla ya jozi 600 za viatu kwa siku ambapo kati ya hizo jozi 450 ni mabuti yanayoweza kutumika kwaajili ya taasisi za ulinzi na usalama na jozi 150 kwaajili ya raia.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mgahama, akipata ufafanuzi kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Magereza, juu ya ramani ya Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, wakati wa kukagua utekelezaji wa Mradi huo unoatekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani, leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani Kilimanjaro.

 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mgahama, akipata maelezo kutoka Meneja Miradi, PSSF juu ya Mpango kazi wa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Viwanda vya ngozi Karanga unoatekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani, wakati wa kukagua mradi huo leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mgahama, akipata ufafanuzi kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Magereza, juu ya ramani ya Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, wakati wa kukagua utekelezaji wa Mradi wa huo unatekelezwa na Mfuko wa PSSSF na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani, leo tarehe 29 Novemba 2019, mkoani Kilimanjaro.